Monday, March 11, 2013

AIRTEL TANZANIA- YADHAMINI MWANAMAKUKA

AIRTEL YADHAMINI TUZO ZA MWANAMAKUKA
Mwenyekiti wa Unit of women Friends Esther (kushoto) akikabidhi Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde cheti cha shukrani kwa Airtel kushiriki na kudhamini tuzo za mwanamakuka kwa mwaka 2013. Akishuhudia ni mtunza fedha Mwate Madinda.*

AMINI NA LINAH KURUDIANA- LOVE WITHOUT COMMITMET

- RECYCLING LOVE IS ALL ABOUT
AMINI AND LINAH-
 
Wasanii wanaotamba katika Muziki wa Kizazi Kipya, Amini na Linah wanatarajia kufufua mahusiano yao upya Machi 17, 2013 ndani ya ukumbi wa Maisha Club jijini Dar es Salaam. Wakizungumza na Kajunason Blog, Amini alisema kuwa ameandaa ma-surprise ya kutosha kwa aliyewahi kuwa mpenzi wake Linah katika kumuonyesha kuwa amerusdi kikamilifu.*

TANZANIA YA PATA BIL 34 KUTAK BENKI YA MAENDELO AFRICA

   
WATER SYSTEM SUPPORT FOR TANZANIA FROM AFRICAN DEVELOPMENT  BANK

BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA YAIPA TANZANIA BIL. 34.8 KWENYE MRADI WA MAJI ZANZIBAR
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam mara baada ya kusaini makubaliano na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wa kuipatia Tanzania shilingi bilioni 34.8 za kusaidia mradi wa maji Zanzibar. Katikati ni Mwakilishi wa AfDB nchini Tonia Kandiero na kulia ni Mtaalam wa Benki hiyo anayeshughulikia masuala ya maji Sabas Marandu.* 

Gazeti la kila siku la kiswahili la Tanzania Daima

1
gazeti la tanzania daima - EzineMark - Free Content Article Directory
4 of Tanzania's Greatest Sights. By: Tom V Powell | 2010-09-20 | Adventure Tourism. It is true decision when you are planning to go on the holiday to tanzania where ...

2
Ijumaa Gazeti
... the udaku wa ijumaa tanzania daima, gazeti sepetu na ijumaa tanzania ijumaa scratch Topic gazeti-la-uwazi ... za mafuriko Firstijumaa gazeti huru la wiki hii la leo, what is ...

3
IPP Media - :: IPPMEDIA
Corruption in Tanzania inching to heights of insanity: It is without doubt that the level of corruption in our country is inching towards new heights of insanity.

4
MATUKIO UK: GAZETI LA UWAZI LEO
Zanzibar Daima....Jana, Leo na Kesho ... SPORAH SHOW TODAY AT 6:PM ON STAR TV TANZANIA ... Ukurasa wa Mbele wa Gazeti la IJUMAA Anaitwa ...

5
MATUKIO UK: GAZETI LA IJUMAA
Zanzibar Daima....Jana, Leo na Kesho ... Story from a young woman lived in Tanzania - East ... Ukurasa wa Mbele wa Gazeti la IJUMAA Anaitwa ...
see more at pul-site

Sunday, January 13, 2013

Gazeti la Mtanzania: kulipa mil 45 kwa BJ Amuli: Kotisoko la kariakoo- gazeti la mtanzania

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemuamuru Mhariri wa gazeti la Mtanzania na Kampuni ya Habari Corporation kumlipa fidia ya jumla ya sh milioni 45 Msanifu wa Majengo ambaye ndiye alichora ramani ya jengo la Soko la Kariakoo Dar es Salaam,Beda Jonathan Amuli kwa kumkashfu kuwa hana taaluma ya usanifu majengo.

Wadaiwa katika kesi hiyo ya madai kashfa Na 29/2008 iliyofunguliwa na Amuli dhidi ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Kariako Kuboja Ng’ungu,Mwariri wa Gazeti la Mtanzania na Kampuni ya Habari Coporation inayochapisha magazeti la Bingwa,The African, Rai,Dimba na Mtanzania ambapo mlalamikaji huyo alikuwa anaomba alipwe sh bilioni tano kama fidia ya kuchafuliwa jina lake kutokana na habari iliyochapishwa na gazeti hilo la Na 4214 la Novemba 23 mwaka 2007 iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho;

“Soko kuu la Kariakoo lipo katikati ya eneo la Kariakoo Dar es Salaam, Kitalu namba 32,limepakana katika maungano ya mitaa mine ya Nyamwezi,Mkunguni, Swahili, Sikuuu na Tandamti. Meneja Mkuu wa Soko ,Kuboja N’ungu anasema mchoro wa jengo hili ulibuniwa na Mtanzania ambaye hakwenda shule kwa ajili ya usanifu wa majengo (Local Architect)anaishi maeneo ya Kigamboni, Dar es Salaam”.

Hukumu hiyo imetolewa hivi karibuni na Jaji Profesa Ibrahim Juma ambapo alisema baada ya kupitia utetezi na vielelezo viliwasilishwa na pande zote mbili amefikia uamuzi wa kukubaliana na hoja za mlalamikaji(Amuli) kwamba habari hiyo ilimshushia heshima, haina ukweli wowote na ili mletea madhara mbele ya jamii kwani habari hiyo ilikuwa ni ya uongo kwani mlalamikaji huyo ni kweli ana taaluma ya usanifu wa majengo na shahada ya usanifu majengo aliipata katika Taasisi ya Teknolojia nchini Israel mwaka 1964.

Jaji Juma alisema mlalamikaji huyo Amuli alifaulu kwa kiwango cha juu kabisa kozi yake hiyo na kwamba ndiye alikuwa Mwafrika wa kwanza toka Tanganyika kupata shahada hiyo ya usanifu majengo na kwamba baada ya kuitimu kozi hiyo msanifu huyo alijiunga na kampuni Zevet International Architect and Engineers of Tel Aviv na kuwa kampuni hiyo ndiyo ilikuwa imeshinda tenda ya kuchora mchoro wa ujenzi wa Hoteli ya Kilamanjaro ambayo sasa inatambulika kwa jina la Kempinski.

Jaji huyo alisema kampuni ya Usanifu Majengo ya ZEVET ilimtuma mlalamikaji (Amuli) jijini Dar es Salaam kama mwakilishi wake ambapo aliweza kusimamia ujenzi wa jengo la iliyokuwa Hoteli ya Kilimanjaro ambapo kampuni ilifanyakazi na mlalamikaji kwa miaka mitano na kisha mlalamikaji alimia katika kampuni nyingine ya usanifu majengo ya BJ AMULI na kwamba moja ya kazi kubwa kampuni hiyo iliyopata ni mradi wa ujenzi wa jengo la Soko la Kariakoo kati ya mwaka 1972-1974 na kisha mlalamikaji ndiye pia aliyechora mchoro wa jengo la Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) na Chuo cha Mafunzo cha Benki ya Taifa ya Biashara(NBC) ambacho kwa sasa ndicho Chuo Kikuu cha Ruaha mkoani Iringa.

“Kwa kazi hizo za usanifu majengo ambazo zilitolewa mahakamani hapa na mdaiwa kama vielelezo kuwa yeye ni msomi wa fani ya usanifu majengo na miongoni mwa kazi alizowahi kuzifanya kupitia taaluma yake ni hizo hapo juu na upande wa wadaiwa wameshindwa kuthibitisha madai ya mlalamikaji ,mahakama hii pia imengalia haki itendeke kwa pande zote mbili licha ni kweli habari hiyo ni kweli ilichapwa na mdaiwa wa pili na wa tatu na likasambazwa mikoa yote ya Tanzania na ni kweli ilimletea usumbufu mlalamikaji…mahakama hii inatoa hukumu ya kukubalina na madai ya mlalamikaji na ina mwamuru mdaiwa wa kwanza na wapili kumlipa fidia ya jumla ya milioni 45 pamoja na riba mlalamikaji kuanzia siku ambayo hukumu hii imesomwa badala ya bilioni tano .”alisema Jaji Profesa Juma.Hukumu imetolewa Mei 5 mwaka 2011.